KAZI YOYOTE YA FASIHI NI ZAO LA JAMII LENGWA
NA Mwl. Msule.
NA Mwl. Msule.
Wamitila,2004:19 ameeleza Fasihi kuwa ni sanaa ya lugha inayoshughulikia
masuala yanayomhusu binadamu matatizo yake, ndoto zake, matumaini yake,migogoro
yake na jinsi anavyoingiliana na mazingira yake. Senkoro F.E
M (2011:11) nae anaeleza kuwa fasihi ni sanaa itoayo maudhui yake kwa kutumia
lugha ya maneno ambayo hutamkwa ama kuandikwa naye Nkwera, Fr.F.V, 2003:94 anafasiri Fasihi ni sanaa yaani mkusanyiko wa kazi mbalimbali
zilizosanifiwa kwa kutumia lugha itumiayo zaidi maneno na kujishughulisha na
jinsi binadamu anavyojitambua mwenyewe binafsi,Pia anavyoathiriwa na binadamu
wenzake aidha na viumbe vingine aina kwa aina katika mazingira mbalimbali ya
maisha.
Kwa ujumla, kutokana na maana za waanishi tofautitofauti
ambao wamejitahidi kutoa maana ya fasihitunaweza kufasili fasihikuwa ni kazi ya
sanaa inayotumia lugha katika njia masimulizi au maandishi katika kufikisha
ujumbe uliokusudiwa kwa jamii husika katika kuikabili mazingira yake katika
nyanja mbalimbali za maisha kamavile siasa uchumi, na utamaduni.
Ndani ya fasihi kama sanaa kuna matawi au tanzu mbili za
fasihi nazo ni fasihi simulizi na fasihi andishi.Fasihi andishi; hii ni fasihi
iliyozuka baada ya kuvumbuliwa kwa mfumo wa maandishi. Huhifadhiwa kwenye
maandishi, ili yasomwe na vizazi vya baadaye. (Wamitila K.W,2004) .Pia wahusika
katika fasihi Andishi hutumia wahusika kama wanadamu, kinyume na fasihi
Simulizi ambayo hutumia wahusika changamano (watu, wanyama, mazimwi n.k).
Fasihi simulizi ni kazi ya sanaa inayotumia lugha, Kazi hii ya sanaa
huhifadhiwa kwa kichwa na kusambazwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo.
(Nchimbi.A.S,2011).Fasihi simulizi ni kazi ya sanaa inayotumia mdomo (tofauti
na maandishi kama fasihi andishi) kama njia kuu maalumu kwa ajili ya kufikisha
ujumbe. Ni sehemu ya msingi ya utamaduni, na vipengere vyake vingi vinafanya
kazi kama katika fasihi kwa ujumla.Pia tunaweza kusema fasihi ni sanaa inayo
jenga taswira ya uhalisi wa maisha ya binadamu hivyo inawasilisha hali,
maingiliano, mivutano na mazingira yake.Hivyo hakuna jamii isiyokuwa na fasihi
kwasababu iliibuka pale jamii ilipoanza kutumia lugha kama chombo cha
mawasiliano
Kwa jumla tunaweza sema kuwa fasihi ni sanaa inayotumia
lugha kueleza maisha na tajirba ya binadamu hasa kwa namna anavyotangamana
binadamu na wenzake pamoja na mazingira yake.
Fasihi ni zao la jamii kwa sabubu zifuatazo;
Fasihi ni zao la jamii kwa sabubu zifuatazo;
Mabadiliko katika jamii,
Mabadiliko katika jamii ni hali ya jamii kubadilika kutoka hatua moja kwenda
hatua nyingine kiuchumi kijamii, kiutamaduni na kisiasa Mabadiliko ya jamii
yana athari kubwa katika fasihi. Fasihi hubadilika pia kutokana na jamii husika
inavyobadilika ili kusawiri mahitaji ya jamii hiyo. Fasihi ni zao la jamii
kwasababu kazi nyingi za kifasihi huzungumzia matukio na kutumia mali ghafi
zinazo patikana katika jamii na siyo ombwe tupu. Mabadiliko yote yaliyo ikumba
jamii ya kitanzania kabla na baada ya uvamizi ndiyo yaliyo amusha hisia za
Penina Muhando kukaa na kuandika tamthiliya yake ya “LinaUbani”. Katika tamthiliya hii mwandishi kwa kiasi kikubwa
ameonesha mabadiliko ya jamii ya kitanzania tangu kabla ya ujio wa uvamizi
ambapo jamii ziliishi kwa amani na mshikamano akitumia kijiji cha Malolo kama
mfano kusawiri jamii zenye amani wakati huo, ameonesha hayo pale anaposema;
“…wenyewetulistarehekulekwetuMalolo.
Chakulakilaaina…” (uk 21).
Pia
anaendelea kuonesha jinsi jamii zilivyo kuwa zikishirikiana katika uzalishaji
pamoja jambo ambalo kazi ya fasihi ilikuwa ni kuhimiza uzalishaji mali.
Anasema;
“…watu wake wengiwema
Kaziwakizichapakwabidiinavicheko
Hakikawalineemeka…” (uk.18)
Ujio
wa wavamizi unabadili mfumo wamaisha wa jamii za kitanzania. Hivyo kazi za
kifasihi za kipindi hiki zilikuwa na maudhui ya kupinga uvamizi huo. Penina
mhando anaonesha jamii ilivyobadilika tangu uvamizi wa kikoloni na utumwa mpaka
kupatikana kwa uhuru uliobadili mfumo wa uongozi kutoka machifu mpaka kuwa na
mfumo rasimi. Mabadiliko haya yalikuwa na athari katika kazi za kifasihi ambazo
zilitungwa kupinga na kusifia viongozi walio leta uhuru kwa jamii.Anasema;
“…ukaja ukoloni,
wazungu wakaja kukaa pale kwetu. Halafu ukoloni ukaisha wazungu wakahama. Ukaja
uhuru wakaondoka machifu. Babu wa baba yako, huyo Daudi akaambiwa wewe siyo
chifu tena…”(uk. 33)
Baadaya
uhuru, Tanzania ilianzisha mfumo wa kijamaa (Azimio la Arusha mwaka 1967) ili
kuinua uchumi. Kazi za fasihi za kipindi hiki zilitungwa kusifu na kupinga
mfumo huu wamaisha. Penina mhando ni miongoni mwa waandishi nguli waloweza
kusawiri madhara ya kuanzishwa kwa mfumo huu hasa katika mpango ya kuwahamisisha
watu katika vijiji miaka ya 1970 haikutekelezwa vyema. Walibomolewa nyumba kama
mhusika Bibi anavyosema;
“…Halafu Kibwana Kata anakuja:”Bomoa!”Tukadhani
anatania. Wakabomoa. Kama vile wanabomoa tutu la kuchezea watoto wadogo!...”(uk.15)
Miaka
ya 1970 Tanzania ilivamiwa na Iddi Amini Dada nakupelekea vita kuibuka. Vita
hii ilisababisha madhara makubwa katika jamii ya kitanzania kiuchumi, kisiasa
na kijamii. Kuporomoka kwa uchumi na vifo vilivyo sababishwa na vita hii
kuliamsha hisia za waandishi wengi kuandika kazi zinazosawiri maisha ya jamii
akiwemo Penina Mhando katika tamthili ya “LinaUbani”.
Fasihi ni zao la jamii kwa sababu husawili yaliyopo katika jamii kama
ifuatavyo;
Wahusika; ni
watu, miti, wanyama, majini, ndege na viumbe vingine vinavyo wakilisha watu
katika kazi ya fasihi ili kuwakilisha hali halisi ya maisha ya watu katika
jamii husika TUKI (1998). Mwandishi wa
kazi ya fasihi hutumia wahusika mbalimbali katika kazi yake ili kusawili na
kuwasilisha mambo mbalimbali yanayotokea katka jamii.Wahusika husawiliwa
kisanaa na mwandishi ili waweze kuwakilisha dhana mbalimbali za maisha katika jamii.Mwandishi husawili mawazo kwa
msomaji kupitia wahusika mawazo na matendo yao mabaya au mazuri katika jamii.Mwandishi
wa tamthiliya ya “LINA UBANI” ametumia wahusika mbalimbali ambao matendo moja
kwa moja yanasawili uhalisia wa maisha ambayo tunayaishi , mfano wa wahusika
hao ni Mtambaji, Bibi,Huila, Sara,
Zoeni,Mota na Mwanahego hawa wametumiwa na mwandishi kama nyenzo ya
kufikisha ujumbe kwa hadhira jamii.Wahusika hawa wameibua dhamira kama vile
matumizi mabaya ya madaraka,matabaka,hali ngumu ya maisha, uwajibikaji, ulevi,
na mapinduzi.Kwenye suala la ulevi na matumizi mabaya ya madaraka Zoeni ameonekana kuwa anatumia vibaya ya
madaraka kutokana na kuwa hakutaka
ushauri wa Huila na hatimaye
kufanya vile anavyojisikia kwakuwa tu hakuna la kumfanya kulingana na ngazi ya
mabarakaka aliyopo nayo.Tukirejelea uk 30 anasema:-
Huila: Hata mimi nina
kazi nyingi lakini hatuwezi kuweka sera ya nishati bila kufuata utaalamu.
Ule mpango wa kufanya
utafiti kuona sehemu gani umeuzima, sasa bila data, bila nini, unaandika sra…
Zoeni: Unanifundisha
kazi?
Huila: Ndiyo ni kazi
yangu kukushauri.
Zoeni: Sihitaji ushauri
wako.Kazi yako ni kutekeleza. (Uk30)
Hii
ndio hali halisi ya jamii zetu kwamba kiongozi katika ngazi ya juu wamekuwa
watu wakutopokea ushauri kutoka kwa watu wa chini juu ya kile wanachojua na
baadae inakuwa tatizo.Hivyo uhusika
mhusika Zoeni umetumika kuonesha ubabe wa viongozi wachache ambao
wanaotumia madaraka vibaya kwa
kutowasikiliza wafanyakazi wenzake kama ilivyokuwa kwa Hulia. Hivyo basi ni
dhahiri kuwa fasihi ni zao la jamii kutoka na kuwa kile kilicho ibuliwa na
mwandishi kinapatikana katika jamii zetu za kiafrika.
wakaona
Borakijijinikumwondoanamjinikumpeleka…”uk5
Mwandishikwakiasikikubwaametumiamandharihalisikutokakatikajamiiya
kitanzaniakuijengakaziyake.Hiiinathibitishakwambafasihinizaolajamiikwani
hutumiamandharizilizopokatikajamii
Mandhari, hii ni sehemu ambayo matukio ya hadithi au
masimulizi hutokea. Madhari yaweza kuwa halisi au ya kubuni .Fasihi ni zao la
jamii kwa sababu mandhari zitumikazo katika hadithi huwa ni mandhari halisi
kutoka katika jamii . Katika tamthilia ya LINA UBANI Mwandishi ameweza kutumia
mandhari halisi kwani mandhari zote zipo katika jamii ya sasa. Kwani amejikita
katika kuelezea mazingira ya kitanzania ambayo ni mazingira baada ya Azimio la
Arusha na vita ya kumwondoa Idi Amin. Tunaona mwandishi anaelezea mandhari ya
Kagera ambapo anaonyesha vita iliyopiganwa huko Kagera.Mfano katika onesho la
kwanza mwandishi anasema
“Bibi: Nikamtafute wapi Daudi
Kagera mimi sikujui mwenzenu…” uk 2
Pia
tunaona mwandishi anatumia mandhari ya mkoa wa Pwani kuelezea mahali walipokuwa
wanapelekwa watumwa mfano katika onesho la tano anasema
“Bibi: Hebu niambie zamani sana ulikuwepo utumwa
Nasikia walikuwa wanapita kijijini kwetu wanapelekwa
Pwani”. Uk 33
Pennina
Mhando ametumia madhari ya ofisini kumuonyesha Zoeni akifanya shughuli
mbalimbali za kiofisi mfano katika onesho lanne anasema
“Ofisini kwa Zoeni, Zoeni yuko
mezani kwake. Mafailikwenye
Kisusu cha “IN”. Kisusu cha “ OUT”linafaili moja…’’uk 27
Katika
jamii ofisi ni sehemu ambayo hutumika kufanya shughuli mbalimbali za kiserikali
na kibinafsi
Pia
mwandishi ameonyesha mandhari ya
nyumbani kwa Huila wakiwa katika majonzi ya msiba na bibi amekaa kwenye mkeka
“Nyumbani kwa Huila. Bibiamekaa kwenye mkeka ameegemea mitomingi…”uk 5
Vilevile
Pennina Mhando ametumia mandhari ya kijijini na mjini pale ambapo bibi
anahamishwa kutoka kijijini kwenye hali ngumu ya maisha na kupelekwa mjini ambapowatu walionekana wakiwa katika
shughuli mbalimbali za maendeleo. Mfano katika onesho la pili mwandishi anasema
“Mtambaji:
Basi masikini bibi yule kilio hakikumwisha wakaona
Bora kijijini kumwondoa na mjini kumpeleka…”uk 5
Mwandishi
kwa kiasi kikubwa ametumia mandhari halisi kutoka katika jamii ya kitanzania
kuijenga kazi yake .Hii inathibitisha kwamba fasihi ni zao la jamii kwani
hutumia mandhari zilizopo katika jamii
Dhamira;
ni ile jumla ya maana anayoivumbua mwandishi
aandikapo na jumla ya maana
anayoitambua msomaji katika usomaji wake
. Dhamira hutumika katik kurejerea mada ya kazi Fulani au ujumbe au mada Fulani
au lengo la kazi hiyo . Kifasihi kuna aina kuu mbili za dhamira yaani dhamira
kuu na ndogondogo . ( Wamitila 2002 ).
Hivyo
basi katika hili ni kweli kuwa fasihi ni zao la jamii kwani kwa kupitia
wahusika huibua dhamira mbali mbali ambalo huibua visa na mabo kadha wa kadha.
Mwandishi katika tamthiliya hii amejadili baadhi ya dhamira mbalimbali kama
vile ,
Uzalendo
ni ile hali ya mtu kupenda nchi yake na kuilinda kwa namna yoyote kama kwa
kumwaga damu . Mfano mwandishi amemtumia Daudi kama mzalendo aliyepigana vita
na kujitoa kadri ya uwezo wake.
Hili
limedhihirika mwandishi anaposema ,
“…….huyo wa pili Daudi
Jeshini kajiunga ,
Kapteni akawa,
Sasa
habari zimefika,
Kule vitani alipo kwenda
Daudi kajifia…..” ( Ukurasa wa 2
).
Hivyo
ni kweli fasihi ni zao la jamii kwani kwa kupitia mambo na matukio yaliyokuepo
katika jamii mwandishi ameweza kuibua
dhamira ya uzalendo ambayo hata sasa
nchini watu husisitizwa zaidi kuwa
wazalendo ilio kulinda amani na mali
zilizopo katika jamii zetu. Pia dhamira
nyingine katika tamthiliya hii ni suala
la uongozi mbaya . Hii ni aina ya uongozi ambayo kiongozi huongoza watu , taifa au mahali Fulani kwa matakwa yake kinyume na utaratibu wa
katiba au mikakati ya kiutawala . Mfano
mwandishi katika tamthiliya hii
ameonyesha suala hili kwa kupitia
muhusika Zoeni . Mwandishi
ameonesha pale Zoeni alipopata kadi za mialiko ya pati anasema ,
“...Kuna
kadi nne nimepata , Pati zenyewe zote
leo. ’’
Huo
ni uongozi mbaya kwani badala ya kujali
majukumu anahitaji kwenda Ujerumani
kuhudhuria pati. Hili ni dhahili kuwa
fasihi ni zao la jamii kwani masuala ya uongozi yapo katika jamii zetu
na ni dhahili uongozi huhitaji
uwajibikaji lakini kutokana na
uzembe wa viongozi hupelekea uongozi
kuonekana mbaya .
Matumizi ya lugha;
Lugha ni chombo cha mawasiliano miongoni mwa jamii , Na matumizi hayo ya lugha
hutofautisha kati ya kazi za kisanaa na isiyo ya kisanaa, Mwandishi wa kazi ya
fasihi hutumia lugha katika kazi yake kuakisi jamii anayo ikusudia, katika
tamthiliya hii mwandishai ametumia lugha vyema katika kuwajenga wahusika wake
Tukianza na jina lenyewe la kitabu "LINA UBANI" Mwandishi anajaribu
kuelezea kuwa japo jamii yake inaonekana kuvunda kwa mwenendo wake na hali
ngumu ya maisha pamoja na matendo ya kiovu yanayofanywa na watu wenye nguvu
kama vile viongozi bado ina nafasi ya kubadilika na kuwa jamii mpya kabisa na
yenye maendeleo na haki kwa kila mwanajamii ukiachana na msemo wa waswahili wa
kuwa "Lakuvunda halina Ubani" Lakuvunda hili la jamii yake lina
ubani.Pia mwandishi Ameweza kutumia
lugha ya kikabila ambayo ni kikaguru .(uk1) tunaona pale bibi anaposema:
Bibi "ing'oma ii sikuidaha doo ae.
woi doo ae
aya .
Nime mwitunda dya mele do".
pia
matumizi ya lugha ya kiswahili ili kumjenga mhusika wake amabye ni muhimu sana
amabye ni Bibi( uk1);
Bibi: ngoma hii siiwezi .oooh! Nisimame juu ya mlima
wa mele.
Jambo hili kwa namna moja limesaidia katika
kuumba hali halisi aliyokuwa nayo Bibi. Pia mwandishi ametumia matumizi ya
tamathali za tabaini, Tabaini ni mtindo
wa uneni wa fasaha ambao msemaji husisitiza kauli kwa kutumia maneno yenye
ukinzani aghalabu neno "si" ambapo tunamsikia Bibi akimlalamikia au
kumsema mtoto wake aliye amua kuolewa na mchusa aliyemweleza ukatili wake kuwa
alikuwa (uk34);
"mbogo
si mbogo, kifaru si kifaru"
Pia
ametumia lugha za kigeni ambazo ni kiigereza,kifaransa na kijerumani katika
kuwajenga wahusika wanaohudhuria mukutano wa kimataifa hali hii inaweka
mazingira ya tamthiliya iwe karibu na uhalisia wa mambo yanayozungumzwa.Hivyo
basi kwa kuangalia matumizi hayo ya lugha ambayo yameaksi kabisa hali halisi ya
jamii , hakuna shaka kuwa fasihi ni zao la jamii.
Kwa
ujumla tunaweza kusema fasihi imekuwa na mchango mkubwa sana katika jamii zetu
kwani ni mambo mengi sana yamefanyika katika jamii. Fasihi imetumika kuonya
lika mbalimbali katika jamii kwa njia ya nyimbo, pia kuelimisha, kurubudisha,
kutunza amali za jamii pia fasihi imeweza kukuza lugha kwani kupitia fasihi
matini nyingi zimeweza kuandikwa na kuweza kuwafikia watu wengi na ata nyingine
kusemwa mbele ya jamii na wana jamii kupata maarifa hayo, hivyo fasihi ni zao
la jamii kwani mambo mengi yanayofanyika katika fasihi yanatokana na jamii
yenyewe..
MAREJELEO
Senkoro.
F.M.M.K (2011). Fasihi. Dar es salaam:
KATTU Limited
Kamusi ya Fasihi: Misingi na Vipengele Vyake. Nairobi: Focus Publications Ltd.
Wamitilia
K.W (2004). Kichocheo cha fasihi simulizi na fasihi andishi, Nairobi: focus, publication. LTD