Jumatano, 19 Juni 2019

FASIHI NI ZAO LA JAMII



KAZI YOYOTE YA FASIHI NI ZAO LA JAMII LENGWA
NA Mwl. Msule.
Wamitila,2004:19 ameeleza Fasihi kuwa ni sanaa ya lugha inayoshughulikia masuala yanayomhusu binadamu matatizo yake, ndoto zake, matumaini yake,migogoro yake na jinsi anavyoingiliana na mazingira yake. Senkoro F.E M (2011:11) nae anaeleza kuwa fasihi ni sanaa itoayo maudhui yake kwa kutumia lugha ya maneno ambayo hutamkwa ama kuandikwa naye Nkwera, Fr.F.V, 2003:94 anafasiri Fasihi ni sanaa yaani mkusanyiko wa kazi mbalimbali zilizosanifiwa kwa kutumia lugha itumiayo zaidi maneno na kujishughulisha na jinsi binadamu anavyojitambua mwenyewe binafsi,Pia anavyoathiriwa na binadamu wenzake aidha na viumbe vingine aina kwa aina katika mazingira mbalimbali ya maisha. 
Kwa ujumla, kutokana na maana za waanishi tofautitofauti ambao wamejitahidi kutoa maana ya fasihitunaweza kufasili fasihikuwa ni kazi ya sanaa inayotumia lugha katika njia masimulizi au maandishi katika kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa jamii husika katika kuikabili mazingira yake katika nyanja mbalimbali za maisha kamavile siasa uchumi, na utamaduni.
Ndani ya fasihi kama sanaa kuna matawi au tanzu mbili za fasihi nazo ni fasihi simulizi na fasihi andishi.Fasihi andishi; hii ni fasihi iliyozuka baada ya kuvumbuliwa kwa mfumo wa maandishi. Huhifadhiwa kwenye maandishi, ili yasomwe na vizazi vya baadaye. (Wamitila K.W,2004) .Pia wahusika katika fasihi Andishi hutumia wahusika kama wanadamu, kinyume na fasihi Simulizi ambayo hutumia wahusika changamano (watu, wanyama, mazimwi n.k). Fasihi simulizi ni kazi ya sanaa inayotumia lugha, Kazi hii ya sanaa huhifadhiwa kwa kichwa na kusambazwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo. (Nchimbi.A.S,2011).Fasihi simulizi ni kazi ya sanaa inayotumia mdomo (tofauti na maandishi kama fasihi andishi) kama njia kuu maalumu kwa ajili ya kufikisha ujumbe. Ni sehemu ya msingi ya utamaduni, na vipengere vyake vingi vinafanya kazi kama katika fasihi kwa ujumla.Pia tunaweza kusema fasihi ni sanaa inayo jenga taswira ya uhalisi wa maisha ya binadamu hivyo inawasilisha hali, maingiliano, mivutano na mazingira yake.Hivyo hakuna jamii isiyokuwa na fasihi kwasababu iliibuka pale jamii ilipoanza kutumia lugha kama chombo cha mawasiliano
Kwa jumla tunaweza sema kuwa fasihi ni sanaa inayotumia lugha kueleza maisha na tajirba ya binadamu hasa kwa namna anavyotangamana binadamu na wenzake pamoja na mazingira yake.
             
  Fasihi ni zao la jamii kwa sabubu zifuatazo;
Mabadiliko katika jamii, Mabadiliko katika jamii ni hali ya jamii kubadilika kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine kiuchumi kijamii, kiutamaduni na kisiasa Mabadiliko ya jamii yana athari kubwa katika fasihi. Fasihi hubadilika pia kutokana na jamii husika inavyobadilika ili kusawiri mahitaji ya jamii hiyo. Fasihi ni zao la jamii kwasababu kazi nyingi za kifasihi huzungumzia matukio na kutumia mali ghafi zinazo patikana katika jamii na siyo ombwe tupu. Mabadiliko yote yaliyo ikumba jamii ya kitanzania kabla na baada ya uvamizi ndiyo yaliyo amusha hisia za Penina Muhando kukaa na kuandika tamthiliya yake ya “LinaUbani”. Katika tamthiliya hii mwandishi kwa kiasi kikubwa ameonesha mabadiliko ya jamii ya kitanzania tangu kabla ya ujio wa uvamizi ambapo jamii ziliishi kwa amani na mshikamano akitumia kijiji cha Malolo kama mfano kusawiri jamii zenye amani wakati huo, ameonesha hayo pale anaposema;
                        “…wenyewetulistarehekulekwetuMalolo. Chakulakilaaina…” (uk 21).
Pia anaendelea kuonesha jinsi jamii zilivyo kuwa zikishirikiana katika uzalishaji pamoja jambo ambalo kazi ya fasihi ilikuwa ni kuhimiza uzalishaji mali. Anasema;
                                     “…watu wake wengiwema
                                    Kaziwakizichapakwabidiinavicheko
                                    Hakikawalineemeka…” (uk.18)
Ujio wa wavamizi unabadili mfumo wamaisha wa jamii za kitanzania. Hivyo kazi za kifasihi za kipindi hiki zilikuwa na maudhui ya kupinga uvamizi huo. Penina mhando anaonesha jamii ilivyobadilika tangu uvamizi wa kikoloni na utumwa mpaka kupatikana kwa uhuru uliobadili mfumo wa uongozi kutoka machifu mpaka kuwa na mfumo rasimi. Mabadiliko haya yalikuwa na athari katika kazi za kifasihi ambazo zilitungwa kupinga na kusifia viongozi walio leta uhuru kwa jamii.Anasema;
“…ukaja ukoloni, wazungu wakaja kukaa pale kwetu. Halafu ukoloni ukaisha wazungu wakahama. Ukaja uhuru wakaondoka machifu. Babu wa baba yako, huyo Daudi akaambiwa wewe siyo chifu tena…”(uk. 33)
Baadaya uhuru, Tanzania ilianzisha mfumo wa kijamaa (Azimio la Arusha mwaka 1967) ili kuinua uchumi. Kazi za fasihi za kipindi hiki zilitungwa kusifu na kupinga mfumo huu wamaisha. Penina mhando ni miongoni mwa waandishi nguli waloweza kusawiri madhara ya kuanzishwa kwa mfumo huu hasa katika mpango ya kuwahamisisha watu katika vijiji miaka ya 1970 haikutekelezwa vyema. Walibomolewa nyumba kama mhusika Bibi anavyosema;
“…Halafu Kibwana Kata anakuja:”Bomoa!”Tukadhani anatania. Wakabomoa. Kama vile wanabomoa tutu la kuchezea watoto wadogo!...”(uk.15)
Miaka ya 1970 Tanzania ilivamiwa na Iddi Amini Dada nakupelekea vita kuibuka. Vita hii ilisababisha madhara makubwa katika jamii ya kitanzania kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kuporomoka kwa uchumi na vifo vilivyo sababishwa na vita hii kuliamsha hisia za waandishi wengi kuandika kazi zinazosawiri maisha ya jamii akiwemo Penina Mhando katika tamthili ya “LinaUbani”. Fasihi ni zao la jamii kwa sababu husawili yaliyopo katika jamii kama ifuatavyo;
Wahusika; ni watu, miti, wanyama, majini, ndege na viumbe vingine vinavyo wakilisha watu katika kazi ya fasihi ili kuwakilisha hali halisi ya maisha ya watu katika jamii husika TUKI (1998).  Mwandishi wa kazi ya fasihi hutumia wahusika mbalimbali katika kazi yake ili kusawili na kuwasilisha mambo mbalimbali yanayotokea katka jamii.Wahusika husawiliwa kisanaa na mwandishi ili waweze kuwakilisha dhana mbalimbali za maisha  katika jamii.Mwandishi husawili mawazo kwa msomaji kupitia   wahusika  mawazo na matendo  yao mabaya au mazuri katika jamii.Mwandishi wa tamthiliya ya “LINA UBANI” ametumia wahusika mbalimbali ambao matendo moja kwa moja yanasawili uhalisia wa maisha ambayo tunayaishi , mfano wa wahusika hao ni Mtambaji, Bibi,Huila, Sara, Zoeni,Mota na Mwanahego hawa wametumiwa na mwandishi kama nyenzo ya kufikisha ujumbe kwa hadhira jamii.Wahusika hawa wameibua dhamira kama vile matumizi mabaya ya madaraka,matabaka,hali ngumu ya maisha, uwajibikaji, ulevi, na mapinduzi.Kwenye suala la ulevi na matumizi mabaya ya madaraka  Zoeni ameonekana kuwa anatumia vibaya ya madaraka kutokana na kuwa hakutaka  ushauri wa Huila na  hatimaye kufanya vile anavyojisikia kwakuwa tu hakuna la kumfanya kulingana na ngazi ya mabarakaka aliyopo nayo.Tukirejelea uk 30 anasema:-
Huila: Hata mimi nina kazi nyingi lakini hatuwezi kuweka sera ya nishati bila kufuata utaalamu.
Ule mpango wa kufanya utafiti kuona sehemu gani umeuzima, sasa bila data, bila nini, unaandika sra…
Zoeni: Unanifundisha kazi?
Huila: Ndiyo ni kazi yangu kukushauri.
Zoeni: Sihitaji ushauri wako.Kazi yako ni kutekeleza. (Uk30)
Hii ndio hali halisi ya jamii zetu kwamba kiongozi katika ngazi ya juu wamekuwa watu wakutopokea ushauri kutoka kwa watu wa chini juu ya kile wanachojua na baadae inakuwa tatizo.Hivyo uhusika  mhusika Zoeni umetumika kuonesha ubabe wa viongozi wachache ambao wanaotumia  madaraka vibaya kwa kutowasikiliza wafanyakazi wenzake kama ilivyokuwa kwa Hulia. Hivyo basi ni dhahiri kuwa fasihi ni zao la jamii kutoka na kuwa kile kilicho ibuliwa na mwandishi kinapatikana katika jamii zetu za kiafrika.
wakaona
Borakijijinikumwondoanamjinikumpeleka…”uk5
Mwandishikwakiasikikubwaametumiamandharihalisikutokakatikajamiiya
kitanzaniakuijengakaziyake.Hiiinathibitishakwambafasihinizaolajamiikwani
hutumiamandharizilizopokatikajamii
Mandhari,  hii ni sehemu ambayo matukio ya hadithi au masimulizi hutokea. Madhari yaweza kuwa halisi au ya kubuni .Fasihi ni zao la jamii kwa sababu mandhari zitumikazo katika hadithi huwa ni mandhari halisi kutoka katika jamii . Katika tamthilia ya LINA UBANI Mwandishi ameweza kutumia mandhari halisi kwani mandhari zote zipo katika jamii ya sasa. Kwani amejikita katika kuelezea mazingira ya kitanzania ambayo ni mazingira baada ya Azimio la Arusha na vita ya kumwondoa Idi Amin. Tunaona mwandishi anaelezea mandhari ya Kagera ambapo anaonyesha vita iliyopiganwa huko Kagera.Mfano katika onesho la kwanza mwandishi anasema
                                           “Bibi: Nikamtafute wapi Daudi
                                                 Kagera mimi sikujui mwenzenu…” uk 2
Pia tunaona mwandishi anatumia mandhari ya mkoa wa Pwani kuelezea mahali walipokuwa wanapelekwa watumwa mfano katika onesho la tano anasema
                                             “Bibi: Hebu niambie zamani sana ulikuwepo utumwa
                                               Nasikia walikuwa wanapita kijijini kwetu wanapelekwa
                                                Pwani”. Uk 33
Pennina Mhando ametumia madhari ya ofisini kumuonyesha Zoeni akifanya shughuli mbalimbali za kiofisi mfano katika onesho lanne anasema
                                                  “Ofisini kwa Zoeni, Zoeni  yuko mezani kwake. Mafailikwenye
                                                     Kisusu cha “IN”. Kisusu cha “ OUT”linafaili moja…’’uk 27
Katika jamii ofisi ni sehemu ambayo hutumika kufanya shughuli mbalimbali za kiserikali na kibinafsi
Pia mwandishi ameonyesha mandhari  ya nyumbani kwa Huila wakiwa katika majonzi ya msiba na bibi amekaa kwenye mkeka
                                          “Nyumbani kwa Huila. Bibiamekaa kwenye mkeka ameegemea                                                             mitomingi…”uk 5
Vilevile Pennina Mhando ametumia mandhari ya kijijini na mjini pale ambapo bibi anahamishwa kutoka kijijini kwenye hali ngumu ya maisha na kupelekwa  mjini ambapowatu walionekana wakiwa katika shughuli mbalimbali za maendeleo. Mfano katika onesho la pili mwandishi anasema
                                                “Mtambaji: Basi masikini bibi yule kilio hakikumwisha wakaona
                                                  Bora kijijini kumwondoa na mjini kumpeleka…”uk 5
Mwandishi kwa kiasi kikubwa ametumia mandhari halisi kutoka katika jamii ya kitanzania kuijenga kazi yake .Hii inathibitisha kwamba fasihi ni zao la jamii kwani hutumia mandhari zilizopo katika jamii
Dhamira; ni ile jumla ya maana anayoivumbua mwandishi   aandikapo  na jumla ya maana anayoitambua msomaji  katika usomaji wake . Dhamira hutumika katik kurejerea mada ya kazi Fulani au ujumbe au mada Fulani au lengo la kazi hiyo . Kifasihi kuna aina kuu mbili za dhamira yaani dhamira kuu na ndogondogo . ( Wamitila 2002 ).
Hivyo basi katika hili ni kweli kuwa fasihi ni zao la jamii kwani kwa kupitia wahusika  huibua dhamira mbali mbali  ambalo huibua visa na mabo kadha wa kadha.
Mwandishi  katika tamthiliya hii  amejadili baadhi ya dhamira mbalimbali kama vile ,
Uzalendo ni ile hali ya mtu kupenda nchi yake na kuilinda kwa namna yoyote kama kwa kumwaga damu . Mfano mwandishi amemtumia Daudi kama mzalendo aliyepigana vita na kujitoa kadri ya uwezo wake.
Hili limedhihirika mwandishi anaposema ,
                                                        “…….huyo wa pili Daudi
                                                           Jeshini kajiunga ,
                                                           Kapteni akawa,
                                                           Sasa habari zimefika,
                                                           Kule vitani alipo kwenda
                                                           Daudi kajifia…..”   ( Ukurasa wa 2 ).
Hivyo ni kweli fasihi ni zao la jamii kwani kwa kupitia mambo na matukio yaliyokuepo katika jamii  mwandishi ameweza kuibua dhamira ya uzalendo  ambayo hata sasa nchini watu husisitizwa  zaidi kuwa wazalendo  ilio kulinda amani na mali zilizopo katika jamii zetu. Pia  dhamira nyingine katika tamthiliya hii ni  suala la uongozi mbaya . Hii ni aina ya uongozi ambayo kiongozi huongoza  watu , taifa au mahali Fulani  kwa matakwa yake kinyume na utaratibu wa katiba au  mikakati ya kiutawala . Mfano mwandishi katika tamthiliya hii  ameonyesha suala hili kwa kupitia  muhusika Zoeni . Mwandishi  ameonesha pale  Zoeni  alipopata kadi za mialiko  ya pati anasema ,
                                       “...Kuna kadi nne nimepata , Pati  zenyewe zote leo. ’’
Huo ni uongozi mbaya kwani  badala ya kujali majukumu anahitaji kwenda Ujerumani  kuhudhuria pati. Hili ni dhahili kuwa  fasihi ni zao la jamii kwani masuala ya uongozi yapo katika jamii  zetu  na ni dhahili uongozi huhitaji  uwajibikaji  lakini kutokana na uzembe wa viongozi  hupelekea uongozi kuonekana mbaya .
Matumizi ya lugha; Lugha ni chombo cha mawasiliano miongoni mwa jamii , Na matumizi hayo ya lugha hutofautisha kati ya kazi za kisanaa na isiyo ya kisanaa, Mwandishi wa kazi ya fasihi hutumia lugha katika kazi yake kuakisi jamii anayo ikusudia, katika tamthiliya hii mwandishai ametumia lugha vyema katika kuwajenga wahusika wake Tukianza na jina lenyewe la kitabu "LINA UBANI" Mwandishi anajaribu kuelezea kuwa japo jamii yake inaonekana kuvunda kwa mwenendo wake na hali ngumu ya maisha pamoja na matendo ya kiovu yanayofanywa na watu wenye nguvu kama vile viongozi bado ina nafasi ya kubadilika na kuwa jamii mpya kabisa na yenye maendeleo na haki kwa kila mwanajamii ukiachana na msemo wa waswahili wa kuwa "Lakuvunda halina Ubani" Lakuvunda hili la jamii yake lina ubani.Pia  mwandishi Ameweza kutumia lugha ya kikabila ambayo ni kikaguru .(uk1) tunaona pale bibi anaposema:

Bibi "ing'oma ii sikuidaha doo ae.
 woi doo ae aya .
Nime mwitunda dya mele do".
pia matumizi ya lugha ya kiswahili ili kumjenga mhusika wake amabye ni muhimu sana amabye ni Bibi( uk1);
Bibi: ngoma hii siiwezi .oooh! Nisimame juu ya mlima wa mele.
 Jambo hili kwa namna moja limesaidia katika kuumba hali halisi aliyokuwa nayo Bibi. Pia mwandishi ametumia matumizi ya tamathali za tabaini,  Tabaini ni mtindo wa uneni wa fasaha ambao msemaji husisitiza kauli kwa kutumia maneno yenye ukinzani aghalabu neno "si" ambapo tunamsikia Bibi akimlalamikia au kumsema mtoto wake aliye amua kuolewa na mchusa aliyemweleza ukatili wake kuwa alikuwa (uk34);
                                                   "mbogo si mbogo, kifaru si kifaru"
Pia ametumia lugha za kigeni ambazo ni kiigereza,kifaransa na kijerumani katika kuwajenga wahusika wanaohudhuria mukutano wa kimataifa hali hii inaweka mazingira ya tamthiliya iwe karibu na uhalisia wa mambo yanayozungumzwa.Hivyo basi kwa kuangalia matumizi hayo ya lugha ambayo yameaksi kabisa hali halisi ya jamii , hakuna shaka kuwa fasihi ni zao la jamii.
Kwa ujumla tunaweza kusema fasihi imekuwa na mchango mkubwa sana katika jamii zetu kwani ni mambo mengi sana yamefanyika katika jamii. Fasihi imetumika kuonya lika mbalimbali katika jamii kwa njia ya nyimbo, pia kuelimisha, kurubudisha, kutunza amali za jamii pia fasihi imeweza kukuza lugha kwani kupitia fasihi matini nyingi zimeweza kuandikwa na kuweza kuwafikia watu wengi na ata nyingine kusemwa mbele ya jamii na wana jamii kupata maarifa hayo, hivyo fasihi ni zao la jamii kwani mambo mengi yanayofanyika katika fasihi yanatokana na jamii yenyewe..

 MAREJELEO
 Senkoro. F.M.M.K (2011).  Fasihi. Dar es salaam: KATTU Limited 
Wamitila K.W.(2004).  Kamusi ya Fasihi: Misingi na Vipengele Vyake. Nairobi: Focus      Publications Ltd.
Wamitilia K.W (2004). Kichocheo cha fasihi simulizi na fasihi andishi, Nairobi: focus,       publication. LTD

Featured Post

FASIHI NI ZAO LA JAMII

KAZI YOYOTE YA FASIHI NI ZAO LA JAMII LENGWA NA Mwl. Msule. Wamitila,2004:19 ameeleza Fasihi kuwa ni sanaa ya lugha inayoshughulikia...